Pages

Wednesday, August 31, 2011

Je, ni haki kujichukulia sheria mkononi???


Kijana huyu kahukumiwa kifo na wananchi weenye hasira kwa kuiba kuku mmoja. Toa maoni yako, kama ni haki alivyouwawa kinyama na hatimaye kuchomwa moto. Linganisha na wizi mkubwa unaofanyika maeneo mbalimbali.
  

Tuesday, August 30, 2011

MPENDA UKWELI ( I LIKE TRUTH): MAISHA MAFUPI, MAREFU YAMEAHIDIWA PIA, AMINI YAPO

MPENDA UKWELI ( I LIKE TRUTH): MAISHA MAFUPI, MAREFU YAMEAHIDIWA PIA, AMINI YAPO: Wapendwa, nawasalimu kwa heshima mnazostahili. Wakubwa kwangu "shikamooni", jika langu "salama?" wadogo zangu "hamjambo?" Kama ilivyo jad...
FOR ENGLISH SPEEKERS:-
Hello,
I  greet you all with due respect.
As our tradition,  we need to know others condition.
Do you believe that time comes when there is no asking "how are you? Did you sleep well last night? ... How is your family?"

Those types of greetings will be a histoyr. Please read in the Bible, Revelation 21:3-5. These are not my words, I just quote.
There will be no deaths (as it is today, diseases, aging, crime, and hunger). There will be no reason to mourn, because everything will be new.

The Almighty God, by his personal name JEHOVAH (Psalms 83:18: Exodus 6:3-9), He loves us so much! That is why he created the earth with everything we need.
For example, if you need fruit, you find it in different flavor. Just ask yourself, why not put just one type of fruit?
Variety of food, why? Flavours are different types, as well as color. Other things even without, we could still live, but we would not enjoy life.
Ask yourself again: Did God create everything, then lets us live only for a short time , die and loose them?CONCETRATE

 



Saturday, July 16, 2011

MAISHA MAFUPI, MAREFU YAMEAHIDIWA PIA, AMINI YAPO

Wapendwa,
nawasalimu kwa heshima mnazostahili. Wakubwa kwangu "shikamooni", jika langu "salama?" wadogo zangu "hamjambo?"

Kama ilivyo jadi, kujuliana hali muhimu.
Je, mnaamini kuna wakati unakuja ambapo hakuna kuulizana "hali yako?, ... umelalaje leo?... vipi homa mtoto anaendeleaje?"

Hii si hadithi ya Abunuwasi, kwa kupata uhakika, tafadhali soma katika Biblia, Ufunuo 21:3-5. Hayo si maneno yangu, nimeyanukuu tu.
Hakutakuwa na vifo (kama ilivyo leo, magonjwa, uzee, uhalifu, wala njaa). Hakutakuwa na sababu yoyote ya kuomboleza, sababu mambo yote yatakuwa mapya.

Mwenyezi Mungu, kwa Jina lake binafsi YEHOVA (Zaburi 83:18 ; Kutoka 6:3-9), anatupenda sana!! Ndio maana aliiumba dunia ikiwa na kila kitu tunachokihitaji.
Kwa mfano, ukihitaji matunda, unayapata yenye ladha tofauti tofauti. Hembu jiulize, kwa nini hakuweka tunda aina moja tu?
Chakula kipo cha aina mbalimbali, kwa nini? Harufu zipo za aina mbalimbali, hali kadhalika rangi. Vitu vingine hata kama havingekuwepo, bado tungeishi, bali tusingefurahia maisha.
Jiulize tena, Je, Mungu aliumba vyote hivyo, kisha tuishi muda mchache tu, tufe na kuviacha?
TAFAKARI.