Pages

Wednesday, August 31, 2011

Je, ni haki kujichukulia sheria mkononi???


Kijana huyu kahukumiwa kifo na wananchi weenye hasira kwa kuiba kuku mmoja. Toa maoni yako, kama ni haki alivyouwawa kinyama na hatimaye kuchomwa moto. Linganisha na wizi mkubwa unaofanyika maeneo mbalimbali.
  

1 comment:

  1. Is a bright Monday, Blessed with Joy and Peace.

    "Ni Jumatatu angavu, imebarikiwa kwa furaha na amani"

    Neno la leo:-
    "Mpende jirani yako kama wewe mwenyewe" Mathayo 22:39.

    Upendo huo (agape katika Kigiriki) ni upendo wa kimaadili ambao unahusisha WAJIBU, KANUNI, NA MWENENDO WA HESHIMA, lakini unaweza kuwa mchangamfu na wenye nguvu sana. (1Petro 1:22) Unaonyeshwa kwa maneno na matendo yasiyo ya kichoyo. (1Kor 13:4-7) Kwa sababu upendo ni sifa ya roho takatifu ya Mungu, unawawezesha Wakristo wa kweli kufanya mambo ambayo wengine hawawezi kufanya, kama vile kushinda tofauti za kijamii, kitamaduni, na kisiasa. (Yohana 13:34,35; Wagalatia 5:22) Watu wenye mfano wa kondoo wanaguswa moyo sana wanapoona upendo huo. Kwa mfano, mwanaume fulani kijana Myahudi huko Israel alipohudhuria kwa mara ya kwanza mkutano wa Kikristo, alishangaa sana kuona ndugu Wayahudi na Waarabu wakimwabudu Yehova pamoja. Kwa hiyo, alianza kuhudhuria mikutano kwa ukawaida na akakubali kujifunza Biblia. Je, unawaonyesha ndugu zako upendo huo wa kutoka moyoni? Na je, unajitahidi kuwakaribisha kwa uchangamfu watu wapya kwenye Jumba lenu la Ufalme, bila kufikiria taifa lao, rangi ya ngozi yao, au cheo chao katika jamii? w10 1/15 3:18,19

    ReplyDelete