Pages

Saturday, July 16, 2011

MAISHA MAFUPI, MAREFU YAMEAHIDIWA PIA, AMINI YAPO

Wapendwa,
nawasalimu kwa heshima mnazostahili. Wakubwa kwangu "shikamooni", jika langu "salama?" wadogo zangu "hamjambo?"

Kama ilivyo jadi, kujuliana hali muhimu.
Je, mnaamini kuna wakati unakuja ambapo hakuna kuulizana "hali yako?, ... umelalaje leo?... vipi homa mtoto anaendeleaje?"

Hii si hadithi ya Abunuwasi, kwa kupata uhakika, tafadhali soma katika Biblia, Ufunuo 21:3-5. Hayo si maneno yangu, nimeyanukuu tu.
Hakutakuwa na vifo (kama ilivyo leo, magonjwa, uzee, uhalifu, wala njaa). Hakutakuwa na sababu yoyote ya kuomboleza, sababu mambo yote yatakuwa mapya.

Mwenyezi Mungu, kwa Jina lake binafsi YEHOVA (Zaburi 83:18 ; Kutoka 6:3-9), anatupenda sana!! Ndio maana aliiumba dunia ikiwa na kila kitu tunachokihitaji.
Kwa mfano, ukihitaji matunda, unayapata yenye ladha tofauti tofauti. Hembu jiulize, kwa nini hakuweka tunda aina moja tu?
Chakula kipo cha aina mbalimbali, kwa nini? Harufu zipo za aina mbalimbali, hali kadhalika rangi. Vitu vingine hata kama havingekuwepo, bado tungeishi, bali tusingefurahia maisha.
Jiulize tena, Je, Mungu aliumba vyote hivyo, kisha tuishi muda mchache tu, tufe na kuviacha?
TAFAKARI.